4.5
(62)

Mwalimu ni mtu ambaye huenda shuleni kufunza watoto.

Mwalimu nimpendaye anaitwa mwalimu ****. Yeye hutufunza somo la Kiswahili na somo la jamii. Mwalimu wangu ana nywele ndefu na ni nyeusi ti ti ti. Mwalimu wangu ni mfupi kama nyundo na yeye ni mkali kama simba.

Mwalimu wangu anapenda kuvaa nguo zenye rangi na pia viatu.

Mwalimu wangu ni mzuri sana wakati mwingine lakini ukikosea, yeye huwa mkali. Mwalimu **** hufunza darasa la nne na la tatu. Mwalimu wangu alisema darasa la nne na darasa la tatu wakipita mtihani, atatupa zawadi kama pipi na biskuti.

Mwalimu nimpendaye, yeye huringa kama tausi na yeye ni mwembamba kama sindano. Mwalimu wangu hupenda rangi ya manjano na rangi ya fedha.
Mwalimu nimpendaye yeye hupenda kula vyakula vingi kama vibanzi na nyama ya kuku. Pia yeye hupeda kunywa vinywaji na kula matunda.

Tukisoma somo la jamii, yeye hutufundisha mambo mengi kama vile tunavyo tunza maji, umuhimu wa miti na kadhalika. Pia kwa somo la Kiswahili, yeye hutufunza ngeli, maumbo, rangi na kadhalika.

Mwalimu nimpendaye pia hutufunza tuwe watu wazuri kwenye nchi yetu. Pia hutufunza kwamba tunaweza tukawa watu muhimu kwenye dunia. Mwalimu **** huenda kanisani kushukuru Mungu kwa uhai aliyempa na pia yeye hutuombea tupite mtihani na tuwe watoto watiifu kwa wazazi wetu na walimu.

Mwalimu nimpendaye ana watoto watatu. Mmoja ni mvulana and wawili ni wasichana. Anawapenda sana kama aliyewapata mapacha. Ninampenda sana mwalimu wangu.

Ninaomba Mola ampe miaka na miaka maishani mwale. Pia aweze kuwalea watoto wake. Pia nawaombea Mola amlinde maishani mwake na pia Mungu awalinde watoto wake. Naomba Mola ambariki sana.

How useful was this post?

Click on a star to rate it!

Average rating 4.5 / 5. Vote count: 62

No votes so far! Be the first to rate this post.